Entertainment

Sultana Writen Updates Today’s Episode

Sultana Writen Updates Today’s Episode: Thursday October 27

Part 1:

Bi Ua atauliza Asya ama leo pia atasema amerukwa na akili after amewasikia waKisema wenyewe kuwa alijifungua mtoto wa kike? Asya atasema ni kweli bi Ua alizaa mtoto wa kike. Asya atajitetea na kusema ati wakati bi Ua alitamuka na kusema alizaa mtoto wa kike, Asya alienda kuuliza bi Salama, na bi Salama akasema ni kweli Ua alijifungua mtoto wa kike. Lakini hi

i ni uongo. Asya anataka bi Salama abaki kwa shida tu. Bi Ua atakumbuka akiuliza Asya kama ana wakika hakuzaa mtoto wa kike? Asya akasema mkunga alikuwa pale, kila mtu alikua pale, sasa Ua anataka aambiwe mara ngapi? After flashback, Ua atauliza Asya yeye ni mwanadamu wa aina gani. Yani amemwacha ateseke hii miaka yoote wakati ukweli alikua anajua? Asya atasema pole. Bi Ua atauliza Salama naye atajitetea vipi? Bi Salama aseme nini sasa wakati lawama imetupwa kwake?

Kokan atafika home. Ako na machungu. Ataichukua ile picha ya Sultana, kisha atakumbuka vile alimuokoa, akaungua ndio akapata hilo kovu kwa uso wake. Anafeel pain hadi kwa buruwein lakini atende nini kando na kukubali kuwa penzi halilazimishwi? Kokan ataichoma ile picha sasa huku analia.

Ua ataambia Asya anataka kujua mtoto wake ni nani na yuko wapi. Balaaaaa  bi Ua atamtazama Salama kisha atauliza ni Sultana? Kidogo watasikia Sultana akilia akisema Major anamuumiza. Kumbe Major anamvutia sultana chini. Sada atakuja kusaidia lakini major atamzaba kofi. Ua kuja kusaidia Major atampa kofi na Ua ataanguka kwa stairs hapo nje na kugonga kichwa chini. Bi Ua——-> ni kama ameenda. Sada atamuokota Sultana na kumwambia pole. Jabali naye ameshtuka na kitendo amemfanyia bi Ua.

Fatima atafanya clearance pale walikua wanakaa. Wanafaa waondoke lakini Dida hataki kumfata. Dida anasema ako na mipango yake mwenyewe. Fatima atamuuliza kama ni mpango wa kukutana na JJ? Dida atasema ndio. Fatima ataambia Dida kama ni JJ, atakutana naye sasa hivi juu wanaenda kwa Jabali. Fatima atasema major amempigia simu ako njiani anakuja. So wanafaa kurudi huko.

Upande mwingine bi Ua sijui amezimia ama ndio sasa atakua katuacha. Sultana ataamua kuondoka huku. Jabali ataambia kina Sada waache kumwangalia wamsaidie kumtoa Ua pale. Kidogo Salama atatoka nje akiita sultana. Jabali atamwambia yeye ndiye chanzo ya haya. Jabali amekanya Salama kuingilia maswala ya familia Yale na hasikii. Salama atadai anajaribu tu….lakini major atamkatiza na kumwambia ajaribu kufungua domo lake aone cha mtema Kuni.

Part 2:

Jabali ataanza ku attack bi Salama. Sada ataingilia na kuambia Jabali kama ako na nguvu apigane naye. Sada ataambia Jabali aachane na wanyonge. Apigane naye juu dunia nzima Inajua yeye ndiye adui yake. Sada ataambia Major bi Salama hatoki hapa mpaka apate nafuu. Sada atauliza major anawezaje kuwa katili kwa mwanamke ambaye alikua mpenzi wake? Sada ataambia Major Salama hajawai kuwa mbaya kwake, hajawai mkosea. Salama atasema imetosha. Hataki mtu kumtetea.

Salama ataambia major ataishi kama mnyama hapa ulimwenguni. Atajuta. Bi Salama ataambia major kila siku anamuonya dhidi ya kumtesa sultana. Major atacheka kwa dharau na kudai anaona Sada ashavuruga akili ya Salama. Asya ataambia Major kwa hicho kicheko akumbuke Salama ndiye alimuokoa mkewe pamoja na mwanae JJ, ambaye Jabali hujichocha ni mridhi wake. Jabali ataingia ndani ya nyumba.

Sultana naye aliumizwa mguu. Akiwa njiani, huku analia, kuna watu wa nduthi watamuona. So wataenda kujua shida ni gani. Kisha watamweka Sultana kwa piki piki moja. Yule jamaa aliyembeba Sultana atatoka naye Alafu wenzake watamfata na piki piki zingine. Wataenda moja kwa moja hadi kwa kina kaka huku wanadai major, Major, Major. Kina Babu wako pale watadai kujua nini mbaya. Mzee Moja ataambia Babu mara ya kwanza vijana walikua tayari kuandamana moja kwa moja hadi kwa Major, lakini Babu akakatalia.

Sasa sahii lazima Major ajue kijijini kuna watu vichwa maji kumliko yeye. Maneno atasema anataka kujua nini mbaya hapa. Sultana atasema hawezi jieleza. Kitu wanafaa kufanya ni waondoke waende hadi kwa Major. Babu atasema wawezi enda kwa Major na wanajua kuna hatari. Sultana atasema ameacha Major na hasira nyingine hatari sana. Wakizidi kukaa hapa watampoteza bi Salama. Vijana watasema waendee waendee. Lakini mwanzele atasema hapana, mpaka wajue kilichotokea. Kaka atadai kama ni kuendea wataenda.

Kaka anadai kujua kama JJ anahusika. Maneno atasema hapana, wote wanajua ni muda major hajakua nyumbani. Sultana atasema hawezi danganya. Major yuko, na amemwacha bi Salama huko. Sultana analia akidai mamake hawezani na adhabu ya Major. Mzee moja atasema hawawezi kumpoteza mkunga ambaye Amesaidia kijiji kwa miaka mingi sana. Bibi zao na dada zao watazaa vipi kama mkunga hayuko? Vijana watasema waendee waendee. Kaka atawauliza wazee wanangoja miujiza gani ndio wajue bi Salama ako hatarini? Babu atasema anakubaliana na hawa vijana. Leo Major lazima awajue. Vijana na wazee wengine watasema waendee…huku wanasema hatutaki kunyanyaswaaa. Mwanzele na maneno pia wata join  hatutaki kunyanyaswaaa, hatutaki kunyanyaswaaa. Hata mimi nime join.

Ndio hawa sasa wameamua kama mbaya mbaya, dawa ya moto ni moto. Kama huyu ni Major, basi atajua nguvu zake ni bunduki tu, na bunduki moja haitawaua wanakijiji wote.

Major naye atasema bi Salama aondoke. Lakini Sada atasema Salama hatoki hapa. Sada ataambia Major bi Salama aliletwa na JJ hapa, so wangoje afike ndo aamue. Jabali atasema JJ hana nyumba hapa. Yeye ndiye kusema. Kidogo watasikia wana firimbi movement kule nje. Kikosi kinaongozwa na Kimoda kwa jina la Paulo wa updates  jitu ambalo linaogopwa sana, saaaana na huyu Major. Yani Major akisikia jina Pauloh, huo mkia wake unaenda nyuma yani Major ananiogopa kabisa.

These are the Sultana Writen Updates Today’s Episode.

HAVE MORE?

Send TIPS/Opinion to  news@kenyanewspaper.co.ke You can also find us on Facebook

Kenya Newspaper

Kenya Newspaper is the fasted growing website for Raw News, Entertainment and Gossip

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Don`t copy text!